mercredi 13 février 2013

USA: -Babby BLACK MAMBA :" Tunafanya kazi banaee..."


Bwingi BAHATI a.k.a Babby Black Mamba,Msanii Mrundi anae ishi Arizona/Phoenix MAREKANI (USA) ameongea na safu yetu hii kuwa hivi karibuni (soon) ataachia pini alioshirikiana na Dj Dog bee na Chonge wakiwa pande zile,nyimbo hio niyakuwapa pole Warundi waliopoteza mali zao baada yaku unguwa kwa soko kuu ya Bujumbura. Alitwambia kuwa :" Kuna wimbo nimeufanya na Wasanii ambao niko nao pamoja kwenye  kundi langu la 'BTU' ,wimbo huo unahusu ku unguwa kwa soko kuu ya Bujumbura, yaani ni ujumbe wa rambi rambi tuliotuma tukiwa uku Marekani kwa jamii ya Burundi kutokana na janga hilo la moto. Ilitu uma tukiwa uku,natukaona vizuri tu utowe mchango huo ambao ni muhimu sana kwa wananchi wa nyumbani." Aliongeza nakusema kuwa :" Akipenda mungu ntakuja kutembea Burundi mwezi December,na wimbo huo unaitwa 'POLE' tulio ulitengenezewa B&B Records,utatoka Juma-mosi na video yake."

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire