dimanche 27 janvier 2013

Soko kuu yote ya Bujumbura imeunguwa...

habari za asubuhi mabibi na mabwana, habari hii kutokana na uzito inayo tulipenda kuwafahamisha warundi na wasio kuwa warundi kuwa asubuhi ya leo soko kubwa (Marche central) imeamka inawaka moto,kutokana na baadhi ya watu tuliowakuta nje sokoni walitwambia kuwa nikutokana na shoti ya umeme. Watu sehemu hio ni wengi mno,kila mmoja anakimbilia kuokowa vya kwake.


 Habari tulizozipata punde ni kuwa Viongozi tofauti tofauti wamefika mahali apo kushuhudia hali hio( Ombusman,Raisi wa kwanza na wa pili). Mh Therence SINIYUNGURUZA alizungumza kuwa atautowa ujumbe baada ya moto huo wote kumalizika, wezi walijitokeza na baadhi yao walikamatwa. Soko imeanza ku unguwa rasmi mida ya saa kumi na mbili  na nusu asubuhi (6h30), gari zakuokowa zimejitokeza kwenye sehemu hio zimechelewa,ya kwanza ilikuja inatokea kwenye uwanja wa ndege. hakuna mtu hata mmoja amefariki ila baadhi ya raia waliopoteza wameonekana ku umia na mchoko usiokuwa na mfano maconi mwao.


Uchunguzi wa matokeo ya ku unguwa kwa soko kuu ya Bujumbura  bado unaendelea...

1 commentaire:

  1. dah msiba mkubwa sana inaskitisha jameni.poleni sana ndugu zanguni ALLAH yupo ata wapa kwa nyingine njia.

    RépondreSupprimer