jeudi 23 janvier 2014

Tizama picha za match ya (Burundi-RDC) na Habari za michezo kwa ujumla. ...

Hizi ni baadhi ya picha za mchuano wa jana kati ya Burundi na DRC :
Kwa upande wa habari za mpira wa wavu ( Volley ball) nchini Burundi ,  ratiba  ya tarehe 25 na 26 February , Wiki ya 2  imepangwa ifwatavyo :

Jumaa - mosi :
New Colombe vs GLC , saa Sita ( 12h00 )
Muzinga vs Rukinzo ,saa saba na nusu ( 13h30 )
BUN vs Amical , saa Tisa ( 15h )

Jumaa-pili :

Muzinga vs Spirou ,Saa Tatu asubuhi ( 9h00 )
Les As vs GLC, kati ya saa nne na saa nne na nusu ( 10h à 10h30 )
Rumuri vs BUN , saa Sita ( 12h )


Michuano yote hiyo imepangwa kuchweza kwenye Uwanja wa Wizara ya Vijana , Michezo na Utamaduni .

- Kwa upande mungine , Wacheza soka wawili mashuhuri duniani, wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya ngono na kahaba aliyekuwa na umri mdogo.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi, alisema kwamba,Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich , alimtumia kama zawadi wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.

Naarifiwa Ribbery alimpilia msichana huyo tiketi ya ndege aweze kusafiri kutoka Ujerumani Kuja Ufaransa kumtumbuiza Ribbery wakati wa sherehe hizo.

Alisema kuwa pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema anayecheza soka yake na klabu ya, Real Madrid.

Kahaba huyo alisema kwamba, aliwaambia wawili, hao kuwa alikuwa mtu mzima wakati huo.

Benzema amekanusha madai ya msichana huyo.

Wachezaji hao wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia

- Shiriksho la mchezo wa soka duniani FIFA, limetoa onyo kwa utawala nchini Brazil, kuwa mji wa kusini wa Curitiba huenda ukaondolewa miongoni mwa miji itakayoandaa fainali ya kombe la dunia, kutokana na kuchelewesha kwa shughuli za ujenzi.

Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema kuwa ukarabati katika uwanja huo unaendelea kwa mwendo wa pole sana.

Ametaja suala hilo kama la muhimu na kuwa FIFA itatangaza katika kipindi cha mwezi mmoja ujao ikiwa mji huo wa Curitiba utasalia kama moja ya miji itakayokuwa mwenyeji wa fainali hizo.

Huku ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla ya fainali hizo kuanza viwanja sita kati ya kumi na mbili vinavyohitajika vimekamilika.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire