mardi 12 novembre 2013

Malengo ya IKOH MULTISERVICE nikuleta mabadiliko kwa upande wa Entertainment nchini Burundi...


Muonekano kwa nje wa mahali palieko jengo la ofisi ya IKOH
Asubuhi ya leo nimetembeleya ofisi za IKOH MULTISERVICE zinazopatikana Mjini kati kwenye Jumba maarufu kama RUSCA PLAZA , barabara ya Urafiki (Avenue de l'Amitie) . IKOH ni mmoja kati ya Kampuni inayo shaba yakukuza na kuweka hadharani vipaji vya wanasana nchini kwakushirikiyana nao kwenye project mbali mbali  . Tulipofika ofisini mapokezi yalikuwa mazuri natulipewa bahati yakutembeleya kona zote za ofisi , hebu tizama mwenyewe kupitiya picha :


Baada yakudhuru sehemu mbali mbali za ofisi ya IKOH nilichukuwa kipindi cha dakika chache kuhojiana na ambao niliyo wakuta ofisini na walini jibu vizuri tena kwa busara :

- Mr ABDALLAH : Mimi ndie Manager kwa upande wa mambo yote yanayo usika na uchukuwaji picha (video) kwenye kampuni hii . Yapata sasa kipindi tukiwa na maakazi hapa kiufupi ni kuwa kazi zinakwenda vizuri alhamdulillah ,tumeipata mikataba yakutengeneza video na kuvitengeneza vipindi vyenye level ya kitaifa na kimataifa kama kwa mfano tunasimamiya Project kabambi ya TPF6 (Tusker Project fame 6) sisi ndiyo tunajiusisha nakurekebisha kisha REMA TV inajiusisha nakuonyesha , ni kipindi maridadi kwa wale wanaofwatiliya mashindano hayo nina imani wanakuwa mara kwa mara wanapata uhondo tosha nakuahamu kinachoendeleya. Kinyume na kipindi hicho IKOH inazitengeneza video za hali ya juu , juzi juzi tumeiyachiya video * Nimedata * ya CHRIS D feat Queen Flo nazinginezo zitakufikiyeni hivi karibuni . Hizi ni baadhi ya picha ya video mpya ya Issa Jamal Yoya :

Fahamu vile vile ya kuwa kuna mlolongo wa vipindi vitakavyokuwa vikipeperushwa moja kwa moja kwenye tovuti ya www.ikoh.biz.

- Mr BOTCHUM : Mimi najishughulisha na kitengo cha production kwa upande wa nyimbo zakuskiya (Audio music) , kazi IKOH inayofanya ni kubwa na kasi inayokuja nayo hapana shaka kama imekuja kuyaleta mabadiliko nchini Burundi . Kwenye studio hii nimeshawapokeya wasanii tofauti tofauti wenye hadhi na ujuzi wa hali ya juu kama Kidum japo hajarikodi ila ni hivi karibuni, Big Fizzo, Rally Joe, T max , Yoya , Samantha , Alan Dupri , R Flow , Matabaro Patient , Queen Flo , Shazzy cool nawengineo wengi . Hii inaonyesha ubabe na utendaji kazi mzuri wakuwakusanya na kufanya nao kazi wasanii hao . Hivi karibuni niatakuwa na kazi pevu yakurikodi nyimbo za album Vol 1 ya project * You'll Love Changes * itakayo wakusanya YOYA , T Max na Samantha .

Pichani : Samntha , Mr H na Yoya.

Kama mlivyofwatiliya kupitiya web site yetu , Manager mkuu Mr IKOH alitangaza hadharani kampeni yake mpya inayo malengo yakuleta mabadiliko nchini kwakuanzisha * YOU'LL LOVE THE CHANGES * itakuwa inawa ambatanisha wasanii wa Burundi na kolabo na wasani mbali mbali kwenye kanda ya East afrika mwaka baada ya mwaka .

Kinyume na vitengo hivyo tofauti IKOH MULTISERVICE iko na kitengo cha habari za Burundi , kanda ya africa mashariki na ulimwenguni , IKOH vile vile imejipa jukumu lakuwa karibu sana na Watangazaji kwa shaba yakupeperusha matangazo yake ili ulimwengu mzima wafahamu Burundi kupitiya shughuli nyeti inazofanya ili kuyaleta mabadiliko nchini kupitiya tasnia zinazo lenga utamaduni .

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire