lundi 24 juin 2013

Dar Es Salaam: HUYU NDIO STAR WA BONGO ASIEJALI UNACHOMFIKIRIA WALA KUSEMA KUHUSU YEYE

Hahaaa wacha nianze tu kwa kucheka, maana nilikua nimekaa tu nikawaza makelele ambayo huwa nayasikia juu ya mastar wetu wa bongo, mara hiki mara kile,kupitia magazeti yetu pendwa, radio na television, nikajiuliza licha ya kuwepo na kelele hizo wanaopigiwa kelele wanajali au yanaingilia sikio moja na kutokea lingine?.
kama wapo wasiojali chochote unachowafikiria wala kuwasema ni akina nani hao...swali likatupiwa facebook, na comments zimefika zaidi ya 500, baada ya kuzipitia nikakutana na jina la Wema likiwa limejirudia mara kibao na kumfanya kuwa namba moja kwa wale wasiojali vyovyote utakavyomfikiria wala kumsema akiwa na asilimia takriban 80 ya coments zote.

Majina mengine yaliyoonekana kujitokeza ni pamoja na Elizabeth Michael (lulu) na PHD Hemedi, jina lililonifurahisha sana kuliona ingawa sikutegemea ni pale mmoja alipocomment na kutaja Tanesco.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire