jeudi 21 février 2013

Primus League : Vital'o fc imelala na fasi ya 2 kwenye msimamo wa Primus League...

Leo Jumaa-tano league ya daraja la kwanza Primus imeshika imeingia kwenye wiki yake ya 10,ikiwa imesalia wiki moja ligi igonge ukuta. Timu mbili ambazo ndizo zinawakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya bara la Africa zimejitupa uwanjani nakujinowa vyakutosha ili kukabiliana na timu kutokea Rwanda kwenye duru ya marudiano kati ya tarehe 1,2,3/March/2013. Leo hii kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore tumeshughudia pambano 2 kati ya :

* Saa nane : Vital'o fc 4 - 0 Flamengo Ngagara ( tambwe Amissi alifunga bao tatu pekee yake).
 * saa kumi  : Lydia Ludic bdi Academic 2 - 3 Muzinga.

N.B : Ifahamike ya kwamba kutokana nakujianda vyakutosha kwa michuano ya club bingwa na kombe la shirikisho, timu ya Vital'o fc na LLB Academic kwenye wiki yake ya mwisho zitacheza wiki ijayo,uku match ya mwisho kabisa itachezwa tarehe 10/March kati ya Flamengo - Royal. Vital'o fc itachuwana na Royal Jumaa-mosi tarehe 23/ February mkoani Muramvya , uku LLB kuchuana na Academie tchite Jumaa-pili tarehe 24/February. Baada ya match hizo , Lydia Ludic itajielekeza Rwanda ,Vital'o fc itaipokea Bujumbura timu ya majeshi ya APR. ( APR 1-2 Vital'o fc ; LLB Ac. 1-0 police Fc). Timu zote 4 zilizocheza leo ziko na mchezo umoja wa zaidi kwa timu zingine.

-Ratiba ya wiki ya mwisho :

* Muramvya : Jumaa-mosi : Saa tisa : Royal fc - Vital'o fc
   Bujumbura  : Jumaa-pili   :  Saa kumi : Academie Tchite - LLB
                           Jumaa-mosi :   Atletico olympic - Flambeau de l'Est

Msimamo wa wiki ya 10
----------------------------------
1. Athletico Olympic 20 points +13
2. Vital'o fc 19 points +11 ( + 1 match)
3. Lydia Ludic Bdi Academie 17 points +6 ( + 1 match)
4. Royal fc 16 points +5 
5. Flambeau de l'Est 16 points +5 
6. Muzinga 14 points -6 ( +1 match) 
7. Prince Louis 12 points -2 
8. Messagers 11 points -1
9. Inter stars 9 points -1
10. Academie Tchite 9 points -7
11. Flamengo fc 7 points -11 ( + 1 match)
12. Espoirs 4 points -14

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire