vendredi 8 février 2013

Canada: -Ben Dasvinton :" Tuko jikoni tunapika nyimbo yakuwapa pole Warundi kwa janga laku unguwa kwa soko..."


Msanii Mrundi Ben Dasvinton ambae anaishi CANADA ametufahamisha kuwa mwaka huu wa 2013 anatarajlitufahamisha kwamba yuko na mpango mzima wakurikodi na Wasanii Warundi ambao wanamajina sasa kwaupande wa mziki nchini pale CANADA. Alitwambia kupitia mahojiano mafupi tuliofanya nae kupitia ukurasa wa facebook :" Kwasasa nimeshamaliza kuiweka hazarani pini yangu 'Go hard',kwa muda huu niko najipanga kuitengenezea mazingira mazuri kwa ifanyia RMX ya hio nyimbo na kombaini ya Wasanii wa nyumbani wanao ishi uku nikizungumzia kama Dj Nicolas,Clark (anaimbaga Gospel),Thierry KIJANYA,Ndero David,Papy,BKY nawengineo...nyimbo hio tumeimba kwa nia moja yakuwapa pole Warundi waliopoteza vyakwao baada ya soko kuunguwa." Aliongeza nakusema:" Niko najianda vile vile nakuimalizia malizia album yangu,nafkiri itakuwa tayari mwezi July akipenda Mungu, kati ya nyimbo zitakazo ibeba album kuna moja ntamshirikisha Msanii mwenza Mcmello kama mu wiki mbili atanikuta hapa TORONTO tufanye kazi nae. Nyimbo zangu asilimia 70 (70%) ntatumia umombo (English) kwani kuna bonge la mashindano ntakalo shiriki apa hapa CANADA , kisha baada ya hapo ninampango wakuja kutembea nyumbani mwezi December."

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire