mardi 8 janvier 2013

Rwanda: -Dj Bisoso:"kamwe sintobadili uraia..."Mmoja kati yawa Dj's wanaofanya vizuri kwenye kanda ya Africa mashariki na maziwa makuu Dj BISOSO ambae ni mzaliwa wa mkowani Gitega nchini Burundi,akiwa anazoweleka sana kama Best Dj nchini Rwanda kwa umaarufu ambao kisha jijengea ametufahamisha kupitia mahojiano mafupi tuliefanya nae kuwa :"Mimi natumika Rwanda,natumika na wanyarwanda kama ndugu yao,naishi vizuri,kila Mnyarwanda mahali aliopo anajuwa kuwa nafanya kazi nzuri,nina imani  kuwa kama singelikuwa naweza kamwe nisingelijumuishwa kuyasimamia mashindano ya GUMA GUMA nchini Rwanda na PRIMUSIC nchini Burundi.Ningelipenda kusema kuwa napenda nchi yangu,naniutowe ujumbe kwa wale wote wanaofkiri kuwa ntabadili uraia si abari ya kweli.Siwezi kamwe kusaliti nchi yangu." Ifahamike ya kwamba Dj BISOSO ni mmiliki wa nyumba ya kuchezea mziki usiku ( Night club) inaitwa OLYMPIA. Alifanya kazi nzuri sana kwenye ngazi ya robo fainali Kirundo,nusu fainali Gitega na fainali Jiji kuu Bujumbura apo ni kwa upande wa PRIMUSIC,mashindano yalio malizika kwa ushindi wa Rally joe NIYINZI.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire