jeudi 10 janvier 2013

Fizzo na Olga wapo M.A production,Lolilo ipo Buja Records kwake Liser Classic...

Olga & Fizzo.


Katika shambra shambra zakuanza mwaka kwa vishindo vyakuzitangaza kazi zao,baadhi ya Wasanii nchini wameanza kutembelea tembelea studio tofauti tofauti nakuitaji kuiskia ladhaa ya kazi za ma producers.Mwishoni mwa mwezi wa 12 Big Fizzo aliziacha pini zake 4 (Daima feat Samantha na Mtima wangu feat R Flow akazitengeneza kwa big base-Menya media studio,Ndakumisinze kwa botchum-Ikho multiservice na Nakulove kwake Liser pro-Buja records).
Liser Classic ametupa mgongo,Lolilo yeye akirekebisha sauti ili wakaze beat...


Kinyume na Staa huo,Lolilo alimaliza mwaka naku izinduwa album yake iliosimama na jina 'Mbera umu avocat',kwake binafsi hakuna mdaa wamapumziko niwakati wakuonysha uwezo anao kwakuzitengeneza nyimbo zitazo simama na album yake mwaka huu.Alizungumza kuwa:"Nafkiria kuzitembelea studio tofauti ili nizidi kupata ladha ya kazi zawa producer,na anza na pini 'NACOBIMAZE',ni nyimbo kubwa itakuja kuvunja rikodi ya nyimbo ambazo zilitangulia zilizozungumzia swali lizima la uporaji,ufisadi na maswali kem kem yasio kwenda sambamba na hadhi ya serekali.Washabiki wangu mkae mkao wa kula.",kwa upande mungine Olga Lorie a.k.a Sexy voice ametubainishia kuwa kama mwaka huu wa 2013 atafika mbali zaidi basi ndoto yake itakuwa haijakamilika vizuri,alitwambia kuwa:" Kwa mdaa huu naitaji kuzitowa nyimbo nyingi,zenye ujumbe tofauti wakuijenga nchi yangu,nazingine zakuburudisha.Hivi karibuni pini yangu mimi na Fizzo itakufkieni,itaitwa 'Njo haraka',iko kweye mitindo ya RNB tuko tunaitengenezea kwa M.A production na Amir Mugisha.

1 commentaire: