mardi 24 septembre 2013

Vodacom League : DIDIER Kavumbagu :"Tambwe hanitishi ,nitafunga mengi zaidi kwa vile bado ligi ni mbichi."

KAVUMBAGU akisheherekeya bao lake...


BURUNDI imemtangaza rasmi Amissi Tambwe kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Burundi msimo wa 2012-2013, lakini kasi ya straika huyo mpya wa Simba, imeibua mambo ndani ya Yanga.

Yanga wameanza kumjadili Tambwe huku wengine wakimpuuza na wengine wakimhofia watakapokutana siku thelathini zijazo katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Oktoba 20.

Tambwe alipiga mabao manne Jumatano wiki iliopita ,na juzi kuandikisha mengine mawili na kwasasa kusimama kwenye namba moja kwa upande wawafungaji bora. Tambwe amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga ‘hat trick’ msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa .

Kavumbagu ambaye ni mashine ya mabao Yanga akiongeya na jarida la MWANASPOTI nchini Tanzania, amesema kasi ya Tambwe haimtishi kwani anaamini atafunga mengi zaidi kwa vile bado ligi ni mbichi.

Kavumbagu ambaye amefunga jumla ya mabao matatu alisema: "Siangalii Tambwe amefanya nini, najua kama mabao nitafunga mengi tu, kwa lengo la kuiwezesha Yanga ifanye vizuri lakini si kushindana."

“Hata hivyo ligi bado mbichi, kikubwa kwangu na wachezaji wenzangu ni kukaza buti tu, tupange yajayo na kusahau yaliyopita tutakuwa vizuri tu,” alisema Kavumbagu.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Minziro ametamka kwamba hawafurahii Simba kuongoza ligi na watafanya kila linalowezekana kuishusha.

Minziro alisema: “Kama unavyojua Simba ni wapinzani wetu wakubwa kwenye ligi na wanavyotuacha inauma sana, hali hiyo inatufanya tuhakikishe tunafanya vizuri mechi zijazo tuwakute na kuwapita na naamini mechi ijayo heshima yetu itarudi.”

Tambwe ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Burundi akiwa amefunga mabao 21 wakati klabu yake ya Vital’0 ikimaliza nafasi ya nne. Tambwe aliyejiunga na Simba msimu huu alisema juzi juzi akiongea na jarida la Mwanaspoti : “Ni kweli kwa mara nyingine tena nimekuwa mfungaji bora wa Burundi kwa mabao 21 na nimeambiwa anayenifuatia ana mabao 15."


Matokeo , ratiba ,msimamo na wafungaji bora :

Septemba 21, 2013
Mgambo JKT 1-1 Rhino Rangers (Mkwakwani, Tanga)

Prisons 1-1 Mtibwa Sugar (Sokoine, Mbeya)

Simba SC 2-2 Mbeya City (Taifa, Dar es Salaam)

Kagera Sugar 3-0 Ashanti United (Kaitaba, Kagera)

Septemba 22, 2013

JKT Ruvu 0-1 JKT Oljoro (Azam Complex, Dar es Salaam

Azam FC 3-2 Yanga SC (Taifa, Dar es Salaam)

Coastal Union 1-0 Ruvu Shootings (Mkwakwani, Tanga)

Septemba 25, 2013

Rhino Rangers Vs Ashanti United (A. H. Mwinyi, Tabora)

Septemba 28, 2013

Yanga SC Vs Ruvu Shootings (Taifa, Dar es Salaam)

Rhino Rangers Vs Kagera Sugar (A. H. Mwinyi, Tabora)

Mbeya City Vs Coastal Union (Sokoine, Mbeya)

Mgambo JKT Vs JKT Oljoro (Mkwakwani, Tanga)

Septemba 29, 2013
Ashanti United Vs Mtibwa Sugar (Azam Complex, Dar es Salaam)

JKT Ruvu Vs Simba SC (Taifa, Dar es Salaam)

Prisons Vs Azam FC (Sokoine, Mbeya)

NATIMUPWDLGFGAGDPts
1Simba SC5320134911
2JKT Ruvu53026249
3Coastal Union52305239
4Ruvu Shooting53026339
5Azam FC52308629


Amisi Tambwe/     Simba SC 6

Jerry Tegete / Yanga SC 3

Haruna Chanongo /  Simba SC 3

D. Kavumbangu / Yanga SC 3

Jonas Mkude      /  Simba SC 2

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire