lundi 2 septembre 2013

PRIMUS LEAGUE 2013 :Flambeau de l'Est bingwa wa Burundi kabla ya wiki 1 ligi igonge ukuta...

Picha ya duru ya awali: Lucio na Gatoto walikuwa bado wamo...
Jana kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore ndipo palichezeka mchuano wa katana shoka kati ya Athletico Olympic na Muzinga , mchuano ambao ulikuwa na mvuto wa hali ya juu kulinganisha na uzito wa mchuano huo . Flambeau de l"Est baada ya kwenda sare  ya 0-0 na Academie Tchite siku ya Jumaa-mosi , Lydia Lydic kwenda sare ya 0-0 na Espoir ya Mutimbuzi ambayo itashuka daraja msimo huu , Vital'o Fc kukwamishwa na Messager Ngozi kwa bao 2-0 , timu ya Flambeau de l"Est imeridhika na matokeo hayo ya michuano yote hiyo ikawa imewapa fursa yakutawazwa ubingwa kabla ya wiki 1 ligi kumalizika  kwani iko na hata ikifungwa na Vital'o mchuano wa mwisho itakuwa na alama 1 ya ziada kwa mahasimu wao wanakao mfwata nyuma . Kwa upande wa uongozi huo ni furaha , na hapo jana jioni Tarafani Carama wali itishwa na Kiongozi wao MOISE BUCUMI nakuwashkuru kwa kazi nzuri walio ifanya mwaka mzima . Ni mara ya pili timu ya mikoani kuwa balozi kwenye mashindano ya africa baada ya timu kutokea Kirundo . Ni historia kwa upande wa MUTOMBOLA ,coach wa Flambeau baada yakuipa shavu timu ya LLB kuiwakilisha Burundi miaka 2 kwenye mashindano ya shirikisho na mwaka huu kuitowa bingwa Flambeau . Habari za ndani tulizozipata ni kuwa timu hiyo  maandalizi wataenda kuyafanyika nchini China kwani kuna kampuni ambayo inayowasapoti inayo makaazi pande zile . Hongera sana Flambeau ...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire