lundi 19 août 2013

Primusic 2013 : Wasanii 12 watakao endelea ngazi ya robo fainali kwa upande wa Mea ya Bujumbura...


Tarehe 17 August 2013 tarafani Kanyosha ndipo yalipofanyika mashindano yakuchakachuwa wasanii 12 kinyume na wa 8 kama tulivyowatangazia apo kabla yalifanyika . Jumla ya Wasanii 20 wakiwemo : Amissi Jean alias El Pedro , Bitariho Halidi , Bizimana Tresor , Habonimana Jimmy , Hatangimana Alexis , Inabeza Gladys , Katihabwa Michèle-Samantha , Mabondo Cynthia , Matabaro Patient , Mbazumutima Libère (Cedric Bangy), Nahayo Georges (Memphis) , Nahimana Mick Richard , Nahimana Platini , Ndayishimiye Thomas , Ndayishimiye SADIKI Michel , Ninteretse Jean Marie Christian , Shima Eddy landry , Uwimana Franck , Nshimirimana Richard alias Chrespinho na Vyaribikwiye Jean . Wasanii 12 ndio watakuwa wa balozi wa Mkoa wa Bujumbura kwenye ngazi ya robo fainali itakayofanyika kwenye ukumbi wa shule la SCHEPERS ,tarafani Nyakabiga ifikapo tarehe 24 August . Kwa upande wa tamasha ya leo lakufahamu ni kuwa raia walio itika walikuwa wengi na wakuridhisha ni kitu chakujivunia kwa upnde wa waandalizi wa mashindano hayo,jopo ya wachakachuaji iliongezeka sio wale wa 3 tunao wazowea katika Mikoa mingune tofauti ambayo tayari iliyapokea mashindano hayo kwenye ngazi ya mtoano kwani wanaochaguliwa ni wengi kinyme na Mikoa mingine , walio unda kamati ya Jury kwa leo ilikuwa ni pamoja na ALIDA, Buddy , Arnaud , Amir pro na Steven Sogo . Waliofudhu kuingia kwenye ngazi ya robo fainali ni pamoja na hao wanao onekana kwenye picha hio kama : Amissi Jean alias El Pedro , Bitariho Halidi , Inabeza Gladys , Katihabwa Michèle-Samantha , Mabondo Cynthia , Matabaro Patient , Nahimana Mick Richard , Nahimana Platini , Ndayishimiye Thomas ,Nshimirimana Richard alias Chrespinho...  . Sat b akiwa nyumbani alikonga ile mbaya nyoyo za wapenzi wa mziki wake ,vile vile ilikuwa ni faraja kwa wapenzi wawana muziki ka Mkomboz na Rally Joe bila kuwatenga Top Dance na Black Snakes walio onesha ujuzi wa juu kwakumiliki jukwaa vyakutosha hadi kuacha hoi washabik i. Japo mvua ilipiga kwa wingi siku hiyo ,washabiki hawakujali waliridhishwa nakuendelea nakufurahi bila kujali . Kwa ujumla zowezi  ya kuchakachuwa washindi 12 watakao kuwa wa balozi wa Mea ya Bujumbura haikuwa rahisi kulingana na vipaji vya wasanii waliopambana siku hio,hali ya mshangao kwa wapenzi wa mziki waliohudhuria hapo kuondolewa kwa CEDRIC BANGY mmoja kati ya wakongwe wa mziki wa hapa nchini,kiukweli akustaili kuendelea kutokana na nyimbo alio imba ilikuwa kinyume sana ,nikuweke sawa kuwa ali imba nyimbo ya THE BEN *I'm in love * ,kulingana na mchakachuaji STEVEN SOGO alitowa baada ya huyo kumaliza kuimba kuwa :" Wasanii mnaojulikana ingelikuwa vizuri muwe mnaimba nyimbo zenu kwani mtakapo imba nyimbo za wengine lazima asilimia 80 mumeze sauti na melodi zao ndicho kitu muhimu tunachokiwekea manani sana tunapozigawa pointi " . Tarehe 24/August/2013 moto utawaka kwa upande wa ngazi ya robo fainali. Wait and see...
 Baadhi ya picha :
Jury : SOGO,ARNAUD,ALIDA,AMIR PRO na MZEE BUDDY
Cedric Bangy amevalia nguo nyekundu na weusi,baada yakutangazwa washindi 12...
Mkomboz akiwa jukwani na Papy & Kamanda
Rally Joe akicheza na kundi la Black Snakes.
Sat b jukwani mbele ya halaiki ya raia waliohudhuria...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire