mercredi 28 août 2013

Primusic 2013 : Kampuni ya Brarudi ime endesha Press Conference tarafani Mutanga...

Pichani :Fizzo,Raymond,Mme Aline,Buddy & Denise Gordon.
Kampuni ya vinywaji mbali mbali ya hapa nchini Brarudi , kuptia kitengo cha kinywaji Primus ime endesha mkutano na waandishi habari kutoka kwenye medium tofauti , nia na madhumuni ikiwa ni kumtangaza rasmi mmoja kati ya wakali wa mziki ulimwenguni mwanamama DENISE GORDON ambae amekuja kuwafunza mambo flani flani kuhusikana na kuimba...  wengine wachakachuaji wawili (IRAMBONA Steven Sogo na MUGISHA Amir Pro) watakao shindikiza zoezi hilo lakutowa alama kwa wasanii ambao wamesalia kwenye ngazi ya nusu fainali walitambulishwa . Mwanamama ALINE ambae ndie kiongozi kwa upande wakutangaza biashara (Directrice Marketing)  aliwaonyesha rasmi wasanii wote 12 watakao pambana Jijini Gitega ifikapo Jumaa-pili 1/September/2013 kwenye uwanja wa mpira ,alitangaza mfumo utakao tumiwa kwakufanya uchaguzi kupitia sim za kiganjani kupitia mitandao ya leo,Tempo na hatimae Econet kwakutuma kwenye namba ya 155 . ( Unaandika Primusic kisha una acha nafasi kidogo una andika namba ya msanii unae hitaji kumpa kura yako unapita unatuma kwenye namba hiyo mnamba moja ya sim inaruhusiwa kuchaguwa mara 5 kwa siku ) na web site ya www.primusic.bi inaruhusiwa mara moja kwa siku . Mwisho wa kuchagua ao kuzipana kura itakuwa ni Jumaa-mosi tareh 31/August/2013 saa sita usiku aliongeza mwanamam Aline. Alipochukuwa neno RAYMOND KAMINUZA ,mkuu wa Primusic mwaka huu alijaribu kuweka sawa watangazaji kupitia maswali mbali mbali waliokuwa wanajiuliza kama :

-Kinyume na Msanii MUGANI DESIRE ataongezeka kwenye fainali Msanii kutokea Zambia MAMPI kuja kuongeza utamu kwa wale watakao hudhuria siku hiombila kkusahauvile vile SAT B,Rally joe,MKOMBOZ na T MAX.
-Imeandaliwa tamasha tarehe 8/September/2013 ufukweni kwajitiada zakusaidia wasanii watakao vuka ngazi ya nusu fainali nakuingia kwenye fainali m wale 6 wote wataandaliwa tamasha ufukweni (Plage) ili iwe kwao kama maandalizi tosha ya fainali ya tarehe 14/9/2013 . Ki ingilio siku hio itakuwa ni kununuwa kinywaji mlangoni na hiyo ndio inakuwa kama tiketi ,nia na madhumuni nikukata watu wasiwi wengi sana hadi kusababisha kutolindiwa vyema usalama wao .

- Zawadi zitatolewa ifwatavyo (Prix)  :

1/  15.000.000frsbu

2/  5.000.000frsbu


3/  2.500.000frsbu


4/  1.500.000frsbu


5/  1.000.000frs


6/  500.000frs

- Uchanuzi kupitia sim na web site ulianza jana usiku ,na walipendelea kuruhusu kuandika ujumbe mara tano kwa siku ili kona kiasi gani msanii huo anakavyopendwa na raia, na mara moja kwa upande wa web site ili kuwapa fursa ambao ni wapenzi wa mziki wachague vile vile wanakao wapenda kupitia njia hio.

Namba za wasanii ni hizi zifwatazo :

1. CHRISTIAN
2.GEORGES
3. EL PEDRO
4. LANDRY
5. ALETTA
6. ALAIN MICHEL
7. SAMANTHA
8. GABY
9. OLGA LORIE
10. DOUBLE JAY
11. MATABARO
12. KHALIDY


Baadhi ya picha wakiwa mazoezini :

N.B : Wote kwa jumla wanahitaji kura zenu ili wafahanikishe ndoto zao ...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire