lundi 19 août 2013

Primusic 2013 : Big Fizzo asubiriwa Jumaa-tano hii...( Mercredi soir .)

Mugani Desire a.k.a General Fizzo , Burundiano...


MUGANI DESIRE a.k.a Burundiano , Big Fizzo...Mmoja kati ya wakali wa muziki wa Burundi anae ishi Jijini LILLE  nchini Ufaransa asubiriwa kwa hamu nchini ifikapo siku ya Jumaa-tano usiku na ndege aina ya Bruxelles Airlines . Kwa mujibu wa habari tulizozipata kwa upande wa viongozi wa Primusic 2013 , walitufahamisha  kuwa Msanii huo alipokuwa ziarani Burundi walijaliwa kusaini nae mkataba mungine mwaka huu wa tamasha takribani 4 atakazo ziendesha chini ya uongozi wa Primusic kinyume na zile atakazo ziendesha yeye binafsi kwenye mikataba atakayo ifanya baada ya tarehe 18 /August , tarehe ya fainali ya Primusic 2013 . Ikumbukwe ya kuwa msanii huo mwenye hazi ya ujuzi wakuimba , kuandika nakucheza akiwa kwenye jukwaa amejijengea sifa tele mwaka jana kwenye jumla ya tamasha alizoziendesha kwenye sehemu mbali mbali,alipotoka Burundi nyuma ya mgongo aliacha pini kama : Daima feat Samantha Ndakumisinze, huzuye,Uko wapi , Nakulove ,na ya mwisho kabisa alio acha kwa washabiki wake ikiwa ni * Mama *  . Karibu sana nyumbani...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire