mardi 2 avril 2013

AFRICA NOVA likizoni Burundi baada ya miaka 20 akiwa ukimbizini...
Marie Antoine RUBERINYANGE a.k.a Africanova
yupo Burundi na atamaliza siku 28  baada ya miaka 20 akiwa ukimbizini . Ataendesha Tamasha sehemu mbali mbali Jijini Bujumbura . Mwanamuziki huo ambae sio wakawaida alitikisa Burundi na ulimwengu kupitia nyimbo zake. Hakuna anaeweza kutambuwa kuwa Africanova yuko na miaka 63 . Yuko kwenye foleni ya Wasanii wa enzi zake ambao bado wangali hai , mfano mungine ni Leonce NGABO ambae ana miaka 62 . Tamasha atakazo ziendesha , ni kwa niaba ya mualiko wa Baraza (centre Jean Christophe Matata ) ya hayati Jean Christophe Matata inayo ongozwa na Leonce NGABO .

Kwenye mkutano  na waandishi wa habari ( Journalistes )alio uendesha jana akishindikizwa na Wasanii Serge NKURUNZIZA na Leonce NGABO , Nova alitufahamisha kuwa anarejea kusalimia ndugu Jamaa na marafiki , atachukuwa fursa vile vile yakuendesha Tamasha mbali mbali . Maisha yake yote ni kuimba , fahamu ya kuwa alitunzwa tunzo nyingi barani Africa , Ulaya na Canada . Msanii mkongwe kwenye muziki ali ingia kwenye mambo ya siasa ila kamwe akuheba muziki . Mmoja kati ya Waandishi wa habari walimu uliza kuhusikana nakuchanga siasa na muziki , alijibu kuwa :" Mimi nilibiweza , lakini utajikuta hujipanuwi zaidi kwenye muziki unao ufanya . Ndio maana nilipo ingia kwenye FRODEBU kwa uficho hakuna hata Msanii umoja toka kwenye kundi la (Orchestre) AMABANO niliemshahuri aingie kwenye chama chochote cha siasa . Kipindi hicho tulikuwa tunaimbia UPRONA , tena ata Uganda nilikuwa naimba siasa ." Kwenye Tamasha atakazo ziendesha itakuwa ni fursa nyeti kwake kukutana na nawaimbaji wakizazi kipya ,wazamani ambao bado wangali hai , wapenzi wa kundi lake la zamani la AMABANO . Fahamu ya kuwa Mpendwa msomaji NOVA anaishi Canada toka mwaka 2005 akiwa pamoja na Mkewe na watoto watatu . Karibu sana nyumbani Mzee...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire