vendredi 22 mars 2013

T Max & Big Farious ziarani South africa mwezi mzima (Watasafiri tarehe 10/April...).

Wasanii wawili toka kwenye kundi la Wanajeshi family MUGANI DESIRE a.k.a Big Farious,a.k.a General Fizzo,a.k.a Burundiano na RICHARDS FRANCIS NAMWATA TIMOTHEO a.k.a Colonel T Max,a.k.a Mama...mama Tee , a.k.a Mapafu ya mbwa ifikapo tarehe 10/April/2013 watakuwa wamejielekeza Bondeni (Africa ya Kusini) kwenye ziara ya mwezi mzima . Habari hii ikufkieni nyinyi wasomaji wa blog hii ambao mlikuwa hamninywishi maji , hamchoki kuniuliza kutwa kucha kuhusiana na msafara wa Msanii Farious kuzuru pande za kusini kwa mara yake ya kwanza baada yakuombwa na kombaini ya warundi , wakongomani , wa Tanzania , wa Nigeria , wa zulu na wengi toka nchi mbali mbali aende kule ili ambukizana nao furaha . Hii apa imekuja kukata mzizi wa fitna kwa wale ma Promoters koko, Promoters wenye maneno na wenye kujidai kuwa wanaweza  kumbe hamna lolote...Nikufahamishe mpenzi msomaji kuwa msafara huo umepangwa kwenye tariki hio baada ya Wasanii hao wawili kufanya mkataba na tajiri mrundi anae ishi Jijini Cap Town ambae hakupenda tuliweke hadharani jina lake kwa wasomaji . T Max tulipo jadiliana nae alitufahamisha kuwa :" Faraja kwangu kurudi kwa mara nyingine kwa Mandela Washabiki zangu , makamuzi kwenda mbele...", kwa upande wa Big Fizzo ,yeye anasema kuwa :" Ahadi ni deni , nilikuwa nasema kila siku kuwa pako siku ntatimba pande hizo , akizidi kuniazima pumzi Mwenyezi Mungu , lazima nije uko kwani mambo ya booking ya ndege kwa ajili ya safari ndio tunayo fwatilia hadi mdaa huu kwani mambo yangu nima Aller & Retour nikitumia pipa (Avion) sio yale yakupenya njia za panya , ivo basi naomba watu wa pande zile , wote kwa ujumla wajiandae vyakutosha , mwezi mzima nafkiri tutakinukisha ki jeshi jeshi kweli kweli . Niliahidi mwanzo kama ntakuja ila maelewano yalikuwa madogo kwa wale waliokuwa wananipendekeza mimi kuja huko , makubaliano yalikuwa hafifu . Tunakuja huko kwa Nelson Mandela BADIBA kuchangia furaha nanyi tarehe 10/April/2013 kama kituo kinacho uza tiketi ya ndege South africa hakikubadili msafara wetu .Saluti na salamu za rambi rambi kwa Washabiki wote , nawambia kuwa * Ndabamisinze vya hatari * " . Fahamu kwa mara nyingine  kuwa FARIOUS kwa ushirikiano na mkali wa Show watakuwa 'New Usumbura' 'La Pirogue' ya zamani kwenye Tamasha ijulikanayo kama ' Nakulove Concert' , pini mpia toka kwake T Max inayosimama na jina 'Safari' , miondoko ya hip hop aliotengenezea kwa ADOMIX leo hii ndio ametowa ruhsa yakuchezwa kwenye vituo mbali mbali baada ya kimia kirefu tangu alipotokea Ulaya kwenye maadimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Burundi .  Habari ndio hio...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire