dimanche 3 mars 2013

Champions league : VITAL'O FC 0 - 1 APR (Vital'o itaendelea duru ifwatayo...)

Timu ya Vital'o fc leo hii imelazimishwa mbele ya mashabiki wake bao 1 kwa bila na Timu ya majeshi ya APR kutokea Rwanda, kwenye match ya awali Vital'o ilikuwa imejipatiya ushinde wa bao 2-1, isabu za haraka ni bao 2-2 ila kutoka Vital'o ilijifungia bao nyingi ugenini imepata fursa yakuandikiwa bao 3-2 na kupata fursa yakuendelea mashindano hayo. Burundi mwaka huu imejiandikia historia kwakuzilazimisha timu mbili kutoka Rwanda na hali hii kipindi kirefu ilikuwa haijatokea .Hongera sana Timu zetu kwa hatuwa hio . Ifahamike tu ya kwamba mwezi wa 4 kwa upande wa :
* Champions league : Vital'o fc itacheza na ENOUGOU RANGERS kutokea NIGERIA.
* Confederations Cup : LLB itacheza na Daring Club MOTEMA PEMBE ( DRC).

Orodha ya Wachezaji walio anza pande mbili :


Vital'o fc
------------
25 NDIKUMANA JUSTIN KABENGELE
14 NKURUNZIZA D'AMOUR
8 NKURIKIYE LEOPOLD alias KAYA
19 KAZE GILBERT alias DEMUNGA
15 IDI DJUMAPILI
10 NZIGAMASABO STEVE
11 NDIKUMANA YUSSUF alias LULE
12 ABDALLAH MASSUDI
5 GIRUKWISHAKA JOHN
9 TAMBWE AMISSI

APR FC
-----------
30 NDORI JEAN CLAUDE
13 NSHYUTINAMAGARA ISMAEL
12 RUSHESHONGANGO MICHEL
3 NGABOYISIBO J BOSCO
18 TURATSINZE HERITIER
15 BUTERA ANDREW
7 MUGIRANEZA J BAPTISTE alias MIGI
16 NTAMUHANGA TUMAINE
27 SEKAMANA MAXIME
9 MUBUMBYI BARNABE

Bao pekee la pambano hilo lilipatikana kwenye dakika ya 75' na lilipachikwa kimyani na MUBUMBYI BARNABE baada yakupata pasi muruha toka kwenye winga yakushoto . APR na VITAL'O zote ni kama zimekwenda sawa kwani wameonyesha mpira wakawaida , timu zote mbili zilishambuliana na kosa kosa zilikuwa nyingi kama kwa mfano Mchezaji Deo NDAYISHIMIYE alipo chukuwa na fasi ya JOhn alishindwa kutumia nafasi vizuri kama mbili hivo ,na kwa upande wa APR ilikuwa kama hivo. Burundi mwaka huu kwa upande wa mpira wa miguu hadi mdaa huu inasimama vizuri .  Wabalozi wote ikiwa Vital'o ao LLB na timu ya taifa zote bado zingali mashindanoni,Mungu awaraishiye waendeleye nawafike mbali...
 

1 commentaire:

  1. Felicitation Burundians! So we're waiting for to win Nigeria and it's possible! We invite Judo national team to bring from Zanzibar an East African cup from this 7th championship.

    RépondreSupprimer