mardi 14 janvier 2014

Nyimbo Katoto Remix by Dj Pro feat Mkomboz & Sat b

Mwaka 2014 unaanza vyema kwa msanii mtanashati RAMADHAN KIZA a.k.a Dj Pro baada yakumaliza mwaka 2013 vizuri kwakuachiya bonge la video lililo jijengea sifa kem kem pande zote barani afika hadi ulimwengu mzima.

Dj Pro akichonga na safu yetu ya BB alitufahamisha kuwa :" namshkuru mungu kuona washabiki wangu wanazidi kunipa nguvu nakufarahishwa na kazi nakazo fanya , binanipa nguvu na changamoto kubwa kwakuendeleya nakuheshimu kazi yangu hii nakayofanya ." Aliongeza :" Licha yakuwa na pini mpya *Touch me* niliomshirikishaa Black G
* Touch me *, pini ambayo sijapendeleya kutangaza rasmi kwa washabiki wangu,nina endeleya na kampeni hiyo yakurikodi , jana tarehe 13/1/2014 ndipo nimeingiza sauti kwenye nyimbo yangu mpya inayokwenda na jina la * Katoto remix * , moja kati ya nyimbo iliyonitangaza sana nakuniweka juu , mwanzo nilimshirikisha Franck Gatore Fleury a.k.a Franck Gen80 na Mkomboz , ila hii Remix nimeamuwa kumshirikisha Sat B na Mkomboz , kwa washabiki wangu mkae mkao wa kusubiri... ni soo." fahamu kuwa pini zote hizo mbili zinakarabatiwa buja record's kwa Liser Talent .

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire