mardi 14 janvier 2014

CHAN 2014 : Hizi ndizo pesa wachezaji wa Burundi walizopewa kabla yakujielekeza South afrika.

Photo
Timu ya taifa ya Intamba Murugamba wapo kusini kwa MANDELA , wako Mjini Polokwane na usiku wa leo watamenyane na nchi ya Gabon kwenye mchuano wa kwanza . Burundi tarehe 18/1/2014 itachuana na mauritania , tarehe 22 /1/2014 itapambana na DRC. Idadi ya pesa za burundi zifikazo  454.000frs , sawa na dola 100 kwakuacha nyumbani na laki 3 [300.000frsbu] zilizokusanywa na baadhi ya Viongozi na wapenzi wa soka nchini . Kinyume na hizo , Shirikisho la mpira nchini kwa ushirikiano na Wizara ya vijana michezo na utamaduni wametangaza rasmi kuwa watakuwa wakitowa katika kila mchezo pesa zifikazo dola 50 yaani Wizara kivyake na FFB kivyake kwa mchezaji endapo watafaanikiwa kufunga match (50$ + 50$) . Na wakivuka duru ifwatayo dola 100 kwa kila mchezaji , na ikiwa watavuka duru nyingine pesa watakazopewa zitafaamishwa . Fahamu vile vile ya kuwa idadi ya Dola 300 kwa kila mchezaji iliyokuwa inatolewa imepandishwa hadi dola 500 . Waraka wenyewe ndiyo huu apa :

FFB 001Wachezaji TUYIHIMBAZE Gilbert wa Guepiers du Lac RUGONUMUGABO Stephane wa LLB Academic hakuonekana kwenye picha hizo kwasababu siku walichukuliwa picha hizo hakuwepo mazoezini .

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire