lundi 16 décembre 2013

Filamu "IMPANO" imezinduliwa jana kwenye ukumbi wa OPDE na Kundi la GAME & VISION...

Jana jioni ndipo Shirika la 'Etoile des Réalistes sans Frontières Game & Vision' imeiweka hadharani filamu yao ya nne inayosimama na jina la * IMPANO* baada ya miaka 3 ya nyuma kuziacha kwenye soko filamu tatu zikiwemo * Le dernier Secours, le dialogue na Ubuzima iliyojishindiya tunzo mwaka jana kuwa filamu ya Burundi iliyozingatiya maadili na uboreshaji mwema kwenye mazingira ya teknolojia yakisasa * . Uzinduzi wa filamu hiyo ulifanyika jana baada yakuchelewa kidogo kulingana na muda uliyokuwa umechapishwa kwenye bango , ila hakuchelewa Kiongozi wa Shirika hilo Patrick Amedée kutaka radhi wageni nakuwaomba wawe na moyo wasubira na ndipo paziya zilifunguliwa na burudani kuanza rasmi na msanii wa kizazi kipya ANGELO alieshirikiana na Msanii KOOK KAY kwenye pini yao yenye kutuliya *Beramu* .

Baada ya hao wawili wameivamiya jukwa wasanii watoto wawili kama unao waona kwenye picha hiyo,wasanii hao ambao mmoja aa miaka 5 ungine 6 walimwaga radhi nakuacha watu hoyi kulingana na ujumbe mzito waliyo utowa. badaa ya hao waliyofwata ilikuwa ni Viongozi wa Shirika hilo ambao walichukuwa fursa yakukumbusha walipoanziya na kwasasa wanapofkiya na shaba wanayo katika miaka ya mbele .

Ifahamike ya kuwa kulingana na ratiba ilivyopangwa raia waliyohudhuriya walipata uhondo moja kwa moja kushughudia na kutizama live filamu hiyo inayozungumziya haki ya watoto kwa ujumla na kuwajibika kwa wazazi ili kuwatengenezeya mazingira maridadi kwa maisha yao ya kila siku . Dvd moja inauzwa pesa 10.000 sarafu za Burundi, na niya kama alivyotusimuliya Marie Rose ,naibu kiongozi wa shirikisho hilo :"Siyo kuuza ili turudishe gharama bali nikutaka kuonyesha uwezo wa Burundi kwa upande wa tasniya ya filamu kuwa tunaweza na kuyatowa mafunzo kwa ulemwengu .

Fahamu vile vile ya kuwa filamu hiyo inachukuwa muda wa saa nzima na dakika 34 (1h34min), na  imetafsiriwa na maandishi ya chini kwa kiswahili , kifaransa na kimombo. Jumla ya maswali yadukuduku kwa wapenzi waliyokuwa hapo yalijibiwa na kila aliyekuwa hapo alitowa hoja yake na kwa upande wawaliyoshiriki ilikuwa ni faraja isiyokuwa na mfano kwani biliwasaidiya kufahamu wapi watakosowa wapi wataongeza ili filamu zitakazo fwata ziwe na hadhi yakuridhisha sana. baada ya hapo kwakumaliziya watu waliburudika na kombaini ya wasanii waliyokuwa waalikwa kama DALAX, kundi la ACCENT DU NORD, JOSDY, MAGIC...
 

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire