jeudi 12 septembre 2013

PRIMUSIC 2013 :nani atakaeshinda kati ya OLGA, CHRISTIAN , GABY , EL PEDRO, SAMANTHA na MATABARO ? Fainali ni siku ya Jumaa-mosi 14/09/2013.

Picha tofauti za ujio wa vyombo  vitavyotumiwa kama Jukwaa siku ya fainali ya tayari vimeanza kuunganishwa na hadi Jumaa-mosi  kuwa tayari kutumiwa na Wasanii 6 waliojikatia tiketi ya fainali ( Olga , Matabaro , Samantha , Christian , Gaby na El Pedro ), kinyume na hawo gwaride ndefu ya mziki itadumbwizwa na wasaani tofauti kama JAGUAR kutoka Kenya , Big Fizzo , Sat B , Rally-Joe , Mkomboz , Yvan Muzika , Saidi Brazza , Franck Génération 80 bila kutenda kundi la Black Snakes na TOP  DANCE ... Kumbuka ya kuwa kinyume na mwaka jana Mshindi wa kwanza alinyakuwa Milioni 10 nakurikodi Kenya na KIDUM , mwaka huu washindi wote 6 watatunzwa na wa Kwanza atakusanya pesa Milioni 15 sarafu za burundi .


Kinyume na Jukwaa kuunganishwa nakuwekwa sawa , wasanii na wao kwa ushirikiano tosha na Mwanamama GORDON DENISE wanajikwamuwa vyakutosha pande za Mutanga Nord mahali wanapo endesha kambi yao. Jumla ya asilimia 50 ya Wachakachuaji (Jury ) na asilimia 50 ya ujumbe mfupi wa SMS , mshindi atakae jikusanyia alama (points ) nyingi ndie atakae tawazwa ushindi wa mwaka huu kati ya hao 6 watakao shindana . Kama ilivyokuwa kawaida kila msanii ataimba nyimbo 2 akishindikizwa na kundi la wapigaji alaa (Intsrumentalistes) . Fainali ni siku ya Jumaa-mosi kwenye ukumbi wa EFI NYAKABIGA ,ki ingilio ni pesa 1000frsbu sehemu za kawaida na 5000 frsbu V.I.P.

Zawadi zitakazotolewa :

1/ 15.000.000frs
2/ 5.000.000 frs
3/ 2.500.000 frs
4/ 1.500.000frs
5/ 1.000.000frs 
6/ 500.000frs

N.B : Uchaguzi unaendelea hadi siku ya Ijumaa saa sita usiku ( Vendredi a minuit ), hizi apo chini ni namba wanazotumia kwakuwapa kura ila kinyume na hiyo waweza kuwachaguwa kupitia www.primusic.bi  :

Unaandika neno * primus * unaacha nafasi kisha unatuma kwenda namba 155 kwa wanao tumia mitandao ya Leo, Econet na Tempo .            

1.CHRISTIAN
3. EL PEDRO
7. SAMANTHA
8. GABY
9. OLGA LORIE
11. MATABARO


Baadhi ya picha siku 2 kabla fainali wakiwa mazoezini :

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire