vendredi 9 août 2013

SOGO,YOYA,ROMEO wanaomba mswada wa sheria wakufunga Karaoke urejelewe...

Pichani : Kaposho,Sogo,Romeo & Yoya.
Kwenye uwanja wa Tempete Mjini Bujumbura panapo zoweleka sana kufanyika tamasha mbali mbali maarufu kama KARAOKE ndipo Wasanii wa miondoko ya burundi flava walipokusanya watangazaji na waandishi tofauti kuwaeleza malalamiko yao kuhusiana na mswada wa sheria nambari531.0201/03 wa tarehe 26/1/2011 uliotowa ruhsa ya kutumika kwa shemu zakufurahia (Boite de nuit,karaoke...) na kulinganisha waraka nambari 531.0201/464/CAB/2013 ya tarehe 4/3/2013 Mkuu wa Minisipa ya Mji mkuu Bujumbura ameomba kwa mara ya mwisho wasanii wanao imba karaoke kutozidisha saa mbili usiku. Katikati kwenye barua hio aliandika kuwa :" Yoyote ule atakae hitaji kuanda shughuli hizo lazima aombe ruhsa kwa Mea ya Bujumbura na kwa ujumla yakiwemo mambo yote yanayolingana na ufundi kwenye sehemu hizo. Majumba hayo ambayo hayana mziki lazima yafugwe moja kwa moja,vile vile karaoke ifungwe hadi saa mbili usiku (20h)."
Pichani : Alie wakilisha AMB na Kaposho.


Alionya jopo la usalama la askari polisi la Tarafa ya Rohero kulifanyia kazi swala hilo." Kwa upande wa Wasanii ,kila mmoja aliyatowa malalamiko yake :

* Steven SOGO Irambona  : Binauzunisha sana kuona Msanii anae tangaza nchi yake kwa kazi nzuri anayo ifanye kisha anyanyaswe kwenye nchi yake japo tunapokuwa nje tunathaminika sana. Naomba mswada huo wa sheria alio uwandika Mkuu wa Meya ya Bujumbura afute na pawepo majadiliano na bila kusahau makubaliano yatakayo weka sawa pande zote mbili ili tuone kama tutaishi kwakujivunia kazi yetu hii ya karaoke ambayo kwa kiwango kidogo tunacho kipata tunaridhika nacho. Hiyi ni atuwa ya kwanza,tunataka kuona wapi bitakapo tufkisha endapo jawabu haikupatikana lazima tuombe mikutano ili tueleweshwe vizuri kwani hatuelewi kwanini sisi tunakataliwa ila wengine wanao piga mziki usiku mzima hawakataliwi?

* Romeo Nininahazwe (Etoile du Centre ) : Je! Kuna kazi nyingine walio tuandalia kinyume na hii tunayo ifanya? Mbona ndio inayotuingizia japo kiwango sio kikubwa sana ila inasaidia kwakiasi flani kuendelesha familia zetu. Tuna imba amani,tunasaidia watu wengi kupumzika kichwa kwa shughuli wanazo zifanya wiki nzima,ila leo tuna ambiwa tufunge? Mbona Kanisa haziambiliwi zifunge na zao vile vile zinapiga mziki usiku mzika hadi asubuhi ao wao ni kwasababu wanaimbia Mungu? Kumbe wangelitizama wapi tulipotoka wakati wa vita,wakati walipokuwa wanatuomba tuimbe amani kukusanya watu,leo hii tunapofikia kwa kuidumisha ile amani,na hapo kesho tutakapo kuwa wakati nchi yetu itakapo tambulika zaidi nje ya nchi. Warejeleye mswada huo kwani itakuwa ni kwa manufaa ya warundi wote.

* Yoya Issa Jamal : Nchi inahomba sana endapo shughuli hio haifanyiki nchini. Tizama watumishi wanao tumika wakati jumba flani linafanya karaoke,watumishi wale wana familia zao ambazo zinalishizwa na kazi hizo wanazozifanya! Kwa secta ya utali vile vile tunahomba,msanii atajulikana vipi na raia wanao itembelea Burundi kama hawakuipata fursa yakuitembelea sehemu panapopigwa mziki wakati wa usiku ? Saa mbili inakuwa bado karibu sana,mimi nafkiri ingelikuwa vyema watuongeze hadi saa sita usiku kwani watu wengi mdaa huo unakuwa muafaka kwakwenda kulala.

* Kaposho : Wanatutenga sana,hatuelewi kwanini tunanyanyaswa na huku sisi ndio tunaojulikana kuwa tuko wa balozi wa Burundi kwakudumisha maridhiano,amani na upendo kwa raia kupitia nyimbo zetu? Mswada huo urejelewe kwani sisi wasanii ndio watu tunaotambulika kuwa tunavaa vizuri , vitu vya thamani,sasa ikiwa tunafungiwa kutofanya kazi raia, hususani washabiki zetu watupokeye vipi kesho tukianza kuvaa viraka,haipendezi kwani sisi ni kio cha jamii,kumbe papatikane jawabu maridhawa ya swali hili mapema mno na watuache tufanye kazi kwa amani.

* Amicale des Musiciens : Tumeshangazwa na barua yenyewe,walikuwa wametukubalia mwanzo kuwa watafikisha hadi saa nne (22h) usiku ila tunaskia malalamiko ya wasanii na viongozi wa Bar tofauti tofauti wakilaumu kutokana kuwa wana ambiwa wafunge wakati saa walizo kubaliana hazijatimia. Tunarudi kuombe viongozi wa Minisipa ya Mjii wa Bujumbura walifanyie kazi swala hilo na wawape uhuru wafanye kazi ipasavyo.

1 commentaire: