mercredi 28 août 2013

Exclusive :A$ap Rocky Aamua Kuweka Kila Kitu Wazi Kuhusiana Na Mahusiano Yake Na Rihanna, #Fahamu Zaidi Hapa


Kufuatia rapa A$ap Rocky kuonekana katika pozi za utata na Rihanna hivi karibuni na kufikia hatua ya watu kuanza kufikiri kuwa huenda kuna kitu kimeanza kati yao, Rapa huyu ameamua kufafanua kilichokuwa kinatokea eneo la tukio.

 
A$ap Rocky amesema kuwa hataki kujiingiza katika matatizo ya tetesi kumhusu yeye na Rihanna kwasababu hakuna kitu chochote kinachoendelea kati yao, na yeye na Rihanna ni marafiki wakubwa tu.
 
 
 
Rapa huyu amesema kuwa anampenda Rihanna kwasababu anasapoti kazi zake na hakuna cha ziada, ingawa taarifa za chini chini zinaweka wazi kuwa, Tokea wawili hapa walipofanya tour pamoja, wamejijengea ukaribu wa ajabu ambao unazua maswali mbalimbali kila mara wanapokuwa pamoja.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire