lundi 1 juillet 2013

BIG FARIOUS atupo nae tena Bujumbura...

Fizzo
Msanii wa mitindo yakizamani,yakisasa na inayokuja MUGANI DESIRE a.k.a Burundiano,Farious toka Jumaa-tano iliopita alisafiri kururdi nchini Ufaransa ambapo alienda kukutana kwa mara nyingine na mkeo na mwanae baada ya ziara ya miezi 6 aliokuwa ameizuru Burundi. Farious aliondoka kimya kimya nchini kulingana na roho za kwanini za baadhi ya washabiki washakunaku wasiopenda maendeleo ya wengine.
Mkeo na mwanae...

Msanii kabla yakusafiri alituomba tusitangazi habari yakusafiri kwake hadi atakapo wasili nchini Ufaransa . Kwa yale machache aliotufahamisha kabla yakujielekeza pande zile , alitwambia kuwa :" Mimi nasafiri ila sijapendelea muyatangaze,naomba nitakapo wasili muyaweke wazi ili washabiki na wale wenye roho za husda wafahamu. Nakwenda nikiacha nyuma yangu mambo kibao,nilitengeneza nyimbo za kwangu binafsi kama 8 na kolabo nilizozifanya na wengine wasanii ila kuna baadhi yao maskini ya mungu hatukumaliza,naichukuwa fursa hii kuwaomba samahani soon ntarudi Burundi kushughulikia kandarasi (contrat) nilio saini na Kampuni ya Brarudi kuhusika na mwaka wa pili kwakuyaanda mashindano ya Primusic,ivo basi wasiwe na wasi mambo yote yatakwenda muruwa . Kuhusikana na ahadi nilio itowa ya album (burundiano) bado ipo kwenye mipangilio na akipenda Mungu lazima ni iwakilishe . * Bajou * ni video pekee niliotengeza  na kampuni ya Alfa System,pako zingine zilizokuwa kwenye orodha kama * Ndakumisinze * itakayotoka soon , nikirudi ntatengeneza na Guerra Man ao Producer mungine videos kama Urukumbuzi , Nakulove..." Msanii huo mwenye anao wapenzi wengi nchini na nje ya nchi ali ichukuwa na fasi yakutufahamisha kuwa baada ya pini * Uko wapi* ,amewa achia wapenzi wa nyimbo zake pini mpya inayokwenda na jina la * Maman*. Habari ndio hio...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire