mercredi 18 décembre 2013

CHAN 2014 : Orodha ya Wachezaji 29 wanaojianda michuano hiyo itakayoanza tarehe 11/01/2014.

Baada ya matokeo mabaya yakutovuka ngazi ya robo fainali nchini Kenya kwa upande wa kombe la CECAFA , hii ndiyo orodha ya Wachezaji wanaojinowa tokeya Jumaa-tatu,tarehe 16/12/2013 kwenye uwanja wa mwanamfalme Louis Rwagasore . ifahamike yakuwa kulingana na matayarisho ya Ligi mpya itakayoanza Jumaa-mosi hii tarehe 21/12/2013 Wachezaji hao wanalazimika kufanya mazoezi wakiwa pamoja mara mbili kwa wiki, siku zinazobaki wanasaliya kwenye timu zao , watacheza michuano 5 kabla yakujielekeza Afrika yakusini,kumbuka ya kuwa Burundi itapambana na DRC,Mauritania na Gabon zikiwa kwenye Kundi moja. Jumla ya Wakufunzi wasaidizi 3 wakiwemo Wembo Soutche, Amars NIYONGABO na Mutombola Olivier kwa ushirikano na LOFTI Nassim wanayatowa mafunzo katika siku hizo chache kabla yakujielekeza pande za  kwa Mandela.
Orodha yenyewe ndiyo hii :

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire