lundi 8 avril 2013

South Africa : Big Fizzo na T Max wageni rasmi ndani ya Tamasha 'Buja to South Africa',wataondoka Burundi tarehe 15/4/2013)

Kama tulivyo wafahamisheni wasomaji wa blog hii kuwa MUGANI Desire a.k.a Big Fizzo ao Big Farious na RICHARDS FRANCIS NAMWATA TIMOTHEO a.k.a T Max watajielekeza South Africa kwenye likizo ya mwezi mzima kwa mualiko wawapenzi wa mziki pande zile ni kuwa kinyume nakusafiri tarehe 10 / April /2013 kama tulivyo wajuzeni kabla , Wasanii hao ambao wanasubiriwa kwa hamu pande zile msafara wao umepangwa tarehe 15/ April /2013 . Duru kutoka kwa Africa yakusini kwa wanao anda kila kitu kuhusikana na msafafara wao wametuwekea wazi kuwa wameamuwa kuwapangia Tamasha ya kwanza ifanyike Mjini Cap Town , moja kati ya miji inao Wakimbizi wengi kutoka Burundi wasiokuwa wadogo . Kwa upande wa Fizzo na T Max nilipo hojiana nao waliniwekea wazi kuwa wako tayari na wana imani watawakamuwa ki jeshi jeshi .... Ramadhan Kiza a.k.a Dj Pro mtoto mdogo anae pagawisha raia pande zile ile mbaya kupitia nyimbo zake zenye mvuto na zenye hadhi ya juu atakuwepo kwenye Tamasha hio kama mualikwa akiwa na wengine vijana wanao jichanganya kimziki zaidi . Mpangilio mzima wa show ya kwanza Mjini Cap Town soma kwenye bango (Affiche) apo juu...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire