dimanche 20 janvier 2013

Peter NIYO: " Ndi muto sindi gito"

Msanii wakizazi kipya NIYONGABO Peter Aboubakar mdogo wake na NZIZA Desire Ibrahim(Yupo USA) na YAMUREMYE Claude Abdallah a.k.a Docter Claude ( Yupo Rwanda),Wasanii wawili vigogo waliochafuwa kiwanja cha mitindo ya buja flava miaka ya nyuma kupitia nyimbo zao.Peter NIYO ikiwa ndio jina analolitumia kwenye ngazi hio yakujitangaza nakutangaza kazi zake.Aliongea na safu yetu hii yakupasha habari za tasnia ya mziki nchini kuwa: " Mwaka 2013 ndio huu,ni mdaa muafaka kwa kila Msanii aweze  kujipanga nakujuwa kipi chakufanya ili ajijenge vyakutosha kwenye kazi yake ya mziki.Ki upande wangu sijawa na mengi yakuweka bayana ila Mungu akipenda mwa huu mwezi wa kwanza nta akikisha nimesimama na pini 1 na video 1.Kwa mdaa huu niko natumika nyimbo na Liser Classic nyimbo itaitwa 'Tuzoshika'(Tutafika),mwishoni mwishoni itakuwa tayari...baada ya hio nita acha video yangu 'Pi pi pi' niliotengeneza na Black Arthur chini nembo ya Akaga Videos.Nataka zitokee kwa pamoja zote mbili insha'allah..."Aliongeza nakusema:" (Ndi muto sindi gito...) Mimi bado ningali Msanii mdogo,nina imani yakuwa juu zaidi kwa kazi zangu,na ahidi kujikwamuwa vyakutosha ili miaka ya mbele nifkie kwenye level ya juu...naitaji sapoti yenu washabiki wangu..."Habari ndio hio...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire